“Kutakuwepo na nguvu za hasi na chanya katika maisha yako kadiri utakavyoishi hapa duniani. Ukiruhusu mwili wako utawaliwe na hasi utakuwa hasi. Ukiruhusu mwili wako utawaliwe na chanya utakuwa chanya. Shetani hawezi kuona ndani ya moyo wako hadi wewe wenyewe umwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya uzinzi atakupa uzinzi. Ukionyesha tamaa ya ulevi atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi atakupa wizi, na kadhalika. Kadiri utavyojitahidi kuwa chanya ndivyo utakavyozidi kuwa chanya; na kadiri utavyojitahidi kuwa hasi ndivyo utakavyozidi kuwa hasi. Usipambane na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote dhidi ya Yesu Kristo.” ― Enock Maregesi